FAIDA YA FIQHI

Umuhimu na faida itokanayo na elimu hii ya fiq-hi unajidhihirisha katika maisha ya kila siku ya Muislamu, jamii na ummah mzima wa Kiislamu. Fiq-hi humsaidia Muislamu kujua:-

  • Maamrisho ya Mola wake, akayafuata ikawa ni sababu ya kupatia mafanikio ya Duniani na Akhera.
  • Makatazo ya Mola wake, akayaepuka ikawa pia ndio sababu ya kusalimika na maafa ya Duniani na Akhera.
  • Namna ya kutekeleza lengo la kuumbwa kwake ambalo ni ibada. Vipi na jinsi gani atamuabudu Muumba wake katika maisha yake yote.
  • Uhusiano wake na Mola wake, uhusiano wake na wanadamu wenziwe, uhusiano wa taifa na taifa jingine.
  • Halali na haramu. Fiq-hi ndio humbainishia ni lipi halali kutenda, kusema au kula na ni lipi haramu kutenda, kusema au kula.
  • Hukumu za makosa mbalimbali. Fiq-hi humuongoza Muislamu kutoa hukumu na adabu za makosa mbalimbali kuanzia yale madogo mpaka ya jinai.

Hizi ni baadhi ya faida zipatikanazo katika fani hii ya fiq-hi, kwa kuziangalia na kuzizingatia utaona na kufahamu kuwa Uislamu hauwezi kutekelezeka bila ya kuwa na elimu hii na hapo ndipo unapoonekana umuhimu wa fiq-hi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *