ELIMU / MAARIFA KUINGIA WAKATI WA SWALA

Hii ndio sharti ya pili ya kusihi kwa swala umekwishajua kutokana na maelezo ya darasa zilizotangulia kwamba kila swala ya fardhi ina wakati wake maalum. 

Ili swala  yako isihi ni lazima uiswali ndani ya wakati huo. 

Haitoshi tu kuwa swala inaswaliwa ndani ya wakati kwa sadfa au kubahatisha. 

Bali ni lazima mwenye kutaka kuvaana na swala aijue wakati kupitia elimu/maarifa. 

Hii ni kwa sababu ya kutokusihi kwa swala  ya mwenye kuswali bila ya kujua kuingia itambarikiwa baada ya kumaliza kuswali kuwa amesadifu wakati Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia

“………………… kwa HAKIKA SWALA KWA WAUMINI NI FARDHI ILIYOWEKEWA NYAKATI MAKHSUSI”  4:103.

NAMNA YA KUJUA KUINGIA WAKATI WA SWALA 

NI vipi basi tunaweza kutambua kuwa wakati wa swala fulani umeingia ?  Hili litawezakana kwa kutumia mojawapo ya njia tatu  zifuatazo:-

 1.     maarifa yakinifu:

Mtu atumie dalili hisia (zinazofahamika kupitia milango ya fahamu) kama vile kuliona jua likizama baharini (upande wa bahari)

2.     Jitihada binafsi

Mtu anaweza kutegemea dalili dhahania hizi ni dalili zisizo za moja kwa moja. 

Dalili hizi ni pamoja na kivuli, kipimo cha kazi fulani yaani muda inaochukua kazi hyo. 

Mtu anaweza kusema mathalan kwa kawaida nikianza kushona suruali baada ya adhuhuri mpaka nimaliza huwa ni alasiri tayari.

3.     Kufuata Mjuzi

Itakaposadifu kwamba mtu hana maarifa yakinifu wala hawezi kufanya jitihada binafsi.  

Huyu  ni yule mtu ambaye hazijui nyakati za swala zinaingia saa ngapi na hana maarifa ya kutumia dalili hisia wala dhania kumsaidia kujua wakati wa swala. 

Yeye huyu ina ataamua kumfuata mtu mjuzi mwenye maarifa ua kuingia na kutoka kwa, nyakati za swala kwa kutegemea dalili hisia. 

Akimwambia wakati bado haujaingia basi na asubiri au, atamfuata mtu mwenye kutumia jitihada binafsi kwa kutegemea dalili dhania.

FAIDA:   HUKUMU YA SWALA ILIYOSWALIWA NJE YA WAKATI.

Tunaposema swala iliyoswaliwa nje ya wakati hatumaanishi zaidi ya ile swala iliyosaliwa kabla ya kuingia wakati wake. 

Ni vipi basi  hukumu ya swala hii?   Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu tunasema na il-hali   Yeye ndiye Mjuzi mno. 

Itakapombainikia mtu kwamba swala aliyoiswali;  ameiswali nje ya wakati, yaani kabla ya kuingia wakati wake. 

Kisheria swala hiyo itazingatiwa  kuwa ni  BATILI na ITAMUWAJIBIKIA kuiswali tena ndani ya wakati, bila ya kujali kuwa akiswali kwa kutegemea.

·         Maarifa yakinifu

·         Jitihada binafsi au kwa

·         Kumfuata mjuzi

Swala itakuwa ni batili kwa sababu ya kukosekana sharti mojawapo ya kusihi swala.

ELIMU / MAARIFA KUINGIA WAKATI WA SWALA

Hii ndio sharti ya pili ya kusihi kwa swala umekwishajua kutokana na maelezo ya darasa zilizotangulia kwamba kila swala ya fardhi ina wakati wake maalum. 

Ili swala  yako isihi ni lazima uiswali ndani ya wakati huo. 

Haitoshi tu kuwa swala inaswaliwa ndani ya wakati kwa sadfa au kubahatisha. 

Bali ni lazima mwenye kutaka kuvaana na swala aijue wakati kupitia elimu/maarifa. 

Hii ni kwa sababu ya kutokusihi kwa swala  ya mwenye kuswali bila ya kujua kuingia itambarikiwa baada ya kumaliza kuswali kuwa amesadifu wakati Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *