BARA ARABU WAKATI WA MTUME WAKAZI WAKE

Bara Arabu lipo upande wa kusini wa Bara la Asia. Bara hili ndilo makazi ya Waarabu tangu kale na mpaka sasa kinaishi humo kizazi cha Waarabu.

Maelfu ya miaka Waarabu wa kale wliishi maisha yaliyofanana na maisha yetu ya leo ukiondoa tofauti chache zilizokuwepo.

Walikuwepo miongoni mwao wakazi wa mijini waliostaarabika na kuendelea.

Ama zile tofauti chache zilizokuwepo kati ya maisha ya Waarabu wale wa kale na maisha yetu ya leo ni kwa upande wa kidini (kiitikadi) na kijamii.

Waarabu wa kale waliishi katika enzi/zama za viza zilizotawaliwa na itikadi potofu za kidini na desturi mbaya.

Baada ya kudhihiri Uislamu hali mbaya hizi zilibadilika na Waarabu wakaanza kuishi katika zama za uchanuzi wa dini ya Kiislamu katika mji wa Makkah kisha ikaenea katika pande zote za Bara Arabu Uislamu ulizibadilisha hali na kupigiwa mfano.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *