Ishi na muongozo na maelekezo ya Qur-ani, ufanikiwe duniani na akhera:
Miongoni mwa mambo yanayo pelekea kuongezeka kwa riziki/kipato, ni kukithirisha kuleta Istighfaari: “Nikasema: Ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi, hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe. Atakuleteeni mvua inyeshe mfululizo. Na atakupeni mali na wana, na atakupeni mabustani na atakufanyieni mito”. Nuuhu [71]:10-12