AYA YA WIKI (JUMA LA 80)

ISHI NA MUONGOZO NA MAELEKEZO YA QUR-ANI, UFANIKIWE DUNIANI NA AKHERA

Acha ubishi, Kiyama kinakuja na kipo karibu mno kuliko unavyoweza kufikiria, mche Mola wao:

“Enyi watu! Ikiwa ninyi mna shaka ya kufufuliwa basi kwa hakika Sisi tulikuumbeni kutokana na udongo, kisha kutokana na manii, kisha kutokana na kipande cha damu ilio gandana, kisha kutokana na kipande cha nyama chenye umbo na kisicho na umbo, ili tukubainishieni. Nasi tunakiweka katika matumbo ya uzazi tunacho kitaka mpaka muda ulio wekwa. Kisha tunakutoeni kwa hali ya mtoto mchanga, kisha mfikie kutimia akili. Na wapo katika nyinyi wanao kufa, na wapo katika nyinyi wanao rudishwa kwenye umri wa unyonge kabisa, hata mtu awe hajui kitu baada ya kuwa anakijua. Na unaiona ardhi imetulia kimya, lakini tunapo yateremsha maji juu yake husisimka na kututumka, na kumea kila namna ya mimea mizuri. Hayo ni kwa sababu hakika Allah ndiye Haki, na kwamba hakika Yeye ndiye Mwenye kuhuisha wafu, na kwamba hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu”. Al-Hajji [22]:05-06

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *