AYA YA WIKI (JUMA LA 70)

Ishi na muongozo na maelekezo ya Qur-ani, ufanikiwe duniani na akhera:

Wasia wa Qur-ani kwa wale wote walio timiza umri wa miaka arobaini na kuendelea: “Na tumemuusia mwanaadamu kuwatendea wema wazazi wake wawili. Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu, na akamzaa kwa taabu. Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thelathini. Hata anapo fika utu uzima wake na akafikilia miaka arobaini, aseme: Mola wangu Mlezi! Niwezeshe kushukuru neema zako ulizo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nitende mema unayo yaridhia. Na unitengenezee dhuriya (kizazi) zangu. Hakika mimi nimetubu kwako, na mimi ni miongoni mwa Waislamu”. Al-Ahqaaf [46]:15

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *