AYA YA WIKI (JUMA LA 61)

Ishi na muongozo na maelekezo ya Qur-ani, ufanikiwe duniani na akhera:

Tambua ya kwamba kitabu cha amali zako utakacho pewa siku ya Kiyama, unakiandika mwenyewe kupitia matendo yako, epuka kupewa kitabu chako kwa mkono wa kushoto kwa kutenda leo yanayo mridhi Mola wako: “Na ama atakaye pewa kitabu chake katika mkono wake wa kushoto, basi yeye atasema: Laiti nisingeli pewa kitabu changu! Wala nisingeli jua nini hisabu yangu. Laiti mauti ndio yangeli kuwa ya kunimaliza kabisa. Mali yangu hayakunifaa kitu. Madaraka yangu yamenipotea”. Al-Haqqah [69]:25-29

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *