Ishi na muongozo na maelekezo ya Qur-ani, ufanikiwe duniani na akhera:
Ishi kama atakavyo Mola Muumba wako na si kama yatakavyo matashi na matamanio yako, ili usije kujuta na kusaga meno katika siku ambayo: “Na italetwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini? Aseme: Laiti ningeli itangulizia kwa uhai wangu!”. Al-Fajri [89]:23-24