ADABU / TARATIBU ZINAZOFUNGAMANA NA MAHALA PA KUKIDHIA HAJA

Imemlazimu mkidhi haja, ajiepushe kukidhi haja katika :

1.Njia ya watu au mahala wanapokaa, hii ni kutokana na kero na maudhi yatakayowapata. Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah – Allah amuwie Radhi – kwamba Mtume – Rehma na Amani zimshukie – amesema :

“Yaogopeni mambo mawili yaletayo laana” (Maswahaba) wakauliza : Ni yapi mambo mawili hayo ? (Mtume) akajibu :

“Ni yule ambaye anajisaidia katika njia ya watu au kivuli chao” Muslim.

2. Tundu iliyopo ardhini au ufa wa ukuta/kiambaza.

Hii ni kwa sababu ya kumlinda na kumuepusha mkidhi haja na madhara yanayoweza kumpata.

 Kwani anaweza akawamo ndani ya shimo/ufa mdudu mwenye kudhuru kama vile nge au nyoka, huyu akakerwa na haja akaamua kumtokea mtu na kumdhuru. Imepokelewa kutoka kwa Abdillahi ibn Sarjisi, amesema :

Amekataza Mtume wa Allah – Rehema na Amani zimshukie – kukojoa katika tundu. Abuu Daawood.

3. Chini ya mti utoao matunda.

Hii ni kwa ajili ya kuyahifadhi na kuyalinda matunda yadondokayo yasipatwe na najisi.

Ni mamoja ikiwa matunda hayo yanaliwa au hayaliwi lakini yana manufaa mengine kama dawa.

4. Maji yaliyotuama (yasiokwenda).

Hii ni kutokana na kichefuchefu watumiaji wa maji hayo yakiwa ni mengi yasiyoharibika na najisi na kuyanajisi yakiwa machache na hivyo kuyafanya yasifae kutumika.

Imepokelewa kutoka kwa Jabir – Allah amuwie Radhi – kutoka kwa Mtume – Rehema na Amani zimshukie – kwamba (Mtume) amekataza kukojoa katika maji yaliyotuama”. Muslim.

Kunya ni aula zaidi kwa kukatazwa

 

 

 

ADABU / TARATIBU ZA KUFUATA KATIKA KUKIDHI HAJA NA KUSTANJI (KUCHAMBA)

Sheria imeweka taratibu ambazo muislamu anapaswa kuzichunga na kuzifuata wakati wa kukidhi haja na kustanji. Taratibu hizi tutazigawa katika mafungu/sehemu zifuatazo kama zinavyoelezewa

MAHALA PA KUKIDHIA HAJA

Imemlazimu mkidhi haja, ajiepushe kukidhi haja katika :

1.Njia ya watu au mahala wanapokaa, hii ni kutokana na kero na maudhi yatakayowapata.

(more…)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *