"Dini ni nasaha, wakauliza kwa nani ? Akasema Mtume : Kwa Allah, Mtume wake, kwa viongozi wa waislamu na watu wa kawaida" Hadith Tukufu

MINBARI YA RAMADHANI

Hii ni kutokana na mnasaba wa kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani. Minbari ya Ramadhani itakuwa ikikuletea mawaidha yahusiyanayo na funga ya Ramadhani, ili uweze kuijua funga na hatimaye uweze kufunga kama alivyoamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na kama alivyofunga Bwana Mtume -Rehema na Amani zimshukie - ambaye ndiye kigezo chetu chema. Sambamba na Minbari ya Ramadhani, website yako itakuwa ikikuletea TUNDA LA RAMADHANI.

Kupitia tunda la Ramadhani utajifunza hadithi mbili tatu za Mtume zihusianazo na funga tukufu ya Mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Hadithi hizi zitakuwa zikifuatiwa na maelezo mafupi ili kuziweka wazi kwa wasomaji.