"Mwenyezi Mungu akimtakia kheri Mja humfahamisha (humpa elimu) kwenye dini" Hadith Tukufu

KIKAO CHA MWISHO

Hapa kinachokusudiiwa ni kile kitako kinachokuwa katika rakaa ya   mwisho ya  swala, kinachofandamiwa na salamu.

Ni suna iliyothibiti  kukaa mkao wa “ Tawarruki”  katika kikao hiki cha  mwisho .

Huu ni  mkao ambao mtu hukalia tako la kushoto  na sehemu  ya tako la kulia , akaunyoosha  mguu wa kulia kama unavyokuuwa katika si  jida na kuupitisha ule wa kushoto chini yake.

Imekuja kaatika  riwaya ya Abuu  humayd :

“ ……………..hata ilipokuwa sijida ambayo ndani yake   ndimo imo salamu ( sijida ya mwisho )  huutoa  mguu wake wa  kushoto na akakaa mkao wa tawarruki kwa kukalia tako lake la kushoto” Abuu Daawound