"Mwenyezi Mungu akimtakia kheri Mja humfahamisha (humpa elimu) kwenye dini" Hadith Tukufu

MAANA YA KUSTANJI

Kustanji/Kuchamba ni kusafisha na kuondoa najisi iliyotoka katika mojawapo ya tupu {uchi}mbili au zote mbili; tupu ya mbele na ya nyuma kwa kutumia maji twahara au kinachosimama memo/mahala pa maji wakati wa kukosekana maji kama vile mawe, karatasi, kitambaa, majani na kadhalika.

Mchambaji ahakikishe amejisafisha vema kiasi cha kutobakia athari ya najisi iliyotoka; ikiwa ni mkojo au mavi.

Kustanji/Kuchamba baada ya kukidhi haja ni WAJIBU/FARADHI kama tutakavyoona katika kauli za Mtume – Rehma na Amani zimshukie – katika maelezo yajayo.