KARIBU KATIKA MTANDAO WA UISLAMU

"Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui...." 96:1-5

UTOAJI FATWA

Mwanzoni mwa Uislamu, fat-wa zilikuwa zikitolewa kutoka ndani ya kitabu cha Allah (Qur-ani) na Sunna ya Mtume wake-Rehema na Amani zimshukie-(Hadithi). Na zama hizo nuru ya utume ilikuwa imeuenea uma, walikuwepo wengi miongoni mwao walio zipokea na kuzihifadhi hadithi. Wako walio pokea hadithi nyingi kama walivyo kuwepo wale walio pokea hadithi chache. Miongoni mwa walio pokea hadithi nyingi ni Mama wa Waumini; Bi. Aysha, Abdullah Bin Umar, Abdullah Bin Masoud, Ibn Amrou Bin Al-Aaswi na wengineo-Allah awawiye radhi.

Na zama hizo haikuwepo japo fursa finyu ya kumzulia/kumuongopea/kumsingizia Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-ambalo hakulitenda/hakulisema. Hilo litawezekanaje na ilhali Mtume alikwisha sema: “Atakaye nizulia kwa kukusudia na kwa makusudi, basi na ajichagulie makazi yake motoni”. Bukhaariy [110] & Muslim [03]-Allah awarehemu.

Makhalifa walikuwa wakiwataka fat-wa wale maswahaba wakubwa katika yale matukio yanayo watukia. Sayyidna Umar alipata kumuuliza Abdurahman Bin Auf-Allah awawiye radhi-fat-wa ya mtu aliye muua sungura katika eneo la Haram. Na kwa sababu ya unyeti wa suala la kutoa fat-wa, maswahaba walikuwa wakipeleka mas-ala yanayo hitajia fat-wa kwa wenzao. Pamoja na wingi wao, lakini walio kuwa wakitoa fat-wa hawakuwa wakipindukia kumi na saba. Na hilo lilitokana na kuchelea/kuhofia kwao kutumbukia makosani katika kutoa hukumu.

 

III.            Adhabu za makosa:

         Allah Ataadhamiaye ameweka adhabu kwa matendo mengi ambayo yanaleta fisadi/uharibifu katika uma/jamii. Na adhabu hiyo ni kiondoshi na dhamana ya kutokurejea kuitenda shari/uovu ulio ipasisha adhabu husika. Na adhabu hizo ni za aina nne; kuua (hukumu ya kifo), bakora (kucharazwa bakora), kukata (hukumu ya kukatwa mkono na viungo vingine) na taazira (hukumu ya kuaziriwa). Hebu na tuzitazame aina nne hizi za adhabu, moja baada ya nyingine:

                  1.          KUUA: Hii ni hukumu anayo pitishiwa aliye tenda kosa la:

F         Kumuua mtu pasina haki,

F         Kuritadi (akatoka katika Uislamu),

F         Kueneza fisadi katika ardhi (nchi),

F         Kukimbia katika jihadi,

F         Kuacha swala kwa uvivu, kwa rai moja,

F         Kuzini baada ya kuingia ngomeni (kuoa/kuolewa). Kwa sababu zinaa ni kosa la jinai kwa uma/jamii nzima, kwa kuwa inaharibu utaratibu/mpango wa familia. Akazaliwa kutokana nayo mtoto asiye na baba wa kumlea/kumtunza.

                  2.          BAKORA: Hii ni hukumu inayo tolewa kwa mtu aliye tenda kosa la:

F         Kuzini kabla ya kuingia ngomeni (kuoa/kuolewa), huyu atapigwa bakora mia moja.

F         Kumsingizia mtu kutenda tendo vunda la zinaa, huyu atacharazwa bakora themanini.

F         Kunywa pombe, huyu atatandikwa bakora arobaini au themanini kwa ikhtilafu ya maswahaba katika hilo.

 

                  3.          KUKATA: Hii ni hukumu inayo muangukia yule aliye tenda kosa la:

F         Kuiba (mwizi), huyu atakatwa mkono wake.

Na mtu aliye tenda kosa la jinai lisilo kuua, huyu atachukuliwa kisasi kwa namna na mfano wa alivyo tenda; jicho kwa jicho, pua kwa pua, sikio kwa sikio, jino kwa jino na kwa majaraha kisasi. Na haki ya kusamehe amepewa mtendewa jinai au walii wake.

Ama jinai ikiwa ni kuua na iliyo chini yake, kwa makosa, katika mazingira hayo sheria imemfaradhishia diya (fidia) walii wa mtendewa jinai ya kuuawa. Na kumemstahikia kupata diya katika jinai isiyo kuua, ili iwe katika daraja la badali/malipo ya nafsi au kiungo alicho kipoteza. Na adhabu hii ina faida kwa walio tendewa jinai na ni kemeo kwa watenda jinai.

 

                  4.          TAAZIRA: Hii ni hukumu inayo tolewa kwa makosa yasiyo hayo yaliyo tajwa katika kipengele cha 1 – 3, miongoni mwa makosa yaliyo kanywa na dini. Kama vile kupora, kuacha kufunga (swaumu ya Ramadhani) na yanao fanana na hayo. Haya sheria imeiweka hukumu yake mikononi mwa maliwali, wahukumu kwa mujibu wa mahala na zama.

 

Ingeli kuwa makala yetu haya, maudhui yake ni kuzungumzia tanzu za sheria, basi tunge zielezea hukumu zote za sheria katika adhabu za makosa na masuala ya jinai. Lakini katika mas-ala haya mama tuliyo yataja, ndani yake umo utoshefu wa kuonyesha kwamba utaratibu wa sheria uko juu na ni mtukufu mno kuliko mifumo na taratibu zinazo zuliwa na wanaadamu ambazo hazidumu. Bali hizo kila uchao ziko katika marekebisho na mabadiliko.

Additional information