KARIBU KATIKA MTANDAO WA UISLAMU

"Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui...." 96:1-5

ADHABU YA JARIMA LA KUNYWA ULEVI

“Haddi” ya unywaji wa kilevi, iwe ni tembo (pombe) au kinginecho ni kupigwa mijeledi (bakora) arobaini, kwa sharti tutakazo zitaja. Na kunamjuzia Imamu kuzidisha kiwango hicho mpaka kufikia mijeledi themanini. Na ile iliyo zidi arobaini huwa ni taazira (kuaziriwa/kufedheheshwa) siyo haddi.

 

DALILI YA HILI: Imepokewa kutoka kwa Anas-Allah amuwiye radhi-kwamba Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie: “Alikuwa akipiga katika (unywaji wa pombe) kwa kutumia kuti la mtende na kiatu, (mijeledi) arobaini”. Muslim [1706]-Allah amrehemu.

Na imepokewa (tena) kutoka kwa Anas-Allah amuwiye radhi: “Kwamba Mtume-Rehema na Amani zimshukie-alipiga mijeledi katika (unywaji wa) pombe kwa kutumia (bakora ya) kuti la mtende na kiatu (mijeledi) arobaini. Halafu Abu Bakri-Allah amuwiye radhi-naye akapiga mijeledi arobaini. Alipo shika ukhalifa Umar-Allah amuwiye radhi-na watu wakasogea kutoka mashambani, akauliza: Mna rai gani katika upigaji mijeledi wa pombe? Akasema Abdurahmaan Ibn Auf-Allah amuwiye radhi: Mimi naona ukufanye kama haddi ndogo kuliko zote. Anasema (mpokezi): Umar akapiga mijeledi themanini”.

        Na ikafahamisha kwamba ziada ya arobaini ni taazira, hadithi iliyo pokewa: Kwamba Uthmaan-Allah amuwiye radhi-aliamrisha Al-Waleed Ibn Uqbah Ibn Abi Muaitw apigwe mijeledi. Abdullah Ibn Ja`afar-Allah amuwiye radhi-akampiga mijeledi huku Aliy-Allah amuwiye radhi-akihesabu, mpaka ilipo fika arobaini akasema: Acha (usiendelee kupiga). Halafu akasema: Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-alipiga mijeledi arobaini, na Abu Bakri akapiga arobaini na Umar themanini. Na kila moja ni Sunah, na hii (ya arobaini) inapendeza mno kwangu mimi”. Muslim [1707]-Allah amrehemu.

Mafaqihi-Allah awarehemu-wamesema: Ama arobaini zilizo pokewa kutoka kwa Mtume-Rehema na Amani zimshukie-ndizo haddi (adhabu) ya msingi. Na ama khabari ya kwamba Umar-Allah amuwiye radhi-alipiga mijeledi themanini, wajihi wake ni kama alivyo sema Aliy kumwambia Umar-Allah awawiye radhi wote: “Tunaona upige mijeledi themanini, kwani hakikaye anapo kunywa hulewa na akisha lewa husema hovyo. Na atakapo sema hovyo, huzua (uwongo)”. Maalik [AL-MUWATWAA]-Allah amrehemu.

Na haddi ya uzushi ni kupigwa bakora themanini, na mfano wa hukumu hii, hakika si vinginevyo hutimia taazira. Ni kwa ajili hiyo, ndio ikawa madhehebu ya Imamu Shaafiy-Allah amrehemu-ni kwamba lililo bora ni kukomeka na bakora arobaini, kwani ndizo zilizo pokewa kutoka kwa Mtume-Rehema na Amani zimshukie.

Na wala haddi haitekelezwi kwa mnywaji wa pombe akiwa amelewa, kwa sababu wakati huo haipatikani kwayo makatazo. Hakika si vinginevyo, hungojewa ili azindukane kutoka kwenye ulevi wake, hapo ndipo husimamishiwa haddi. Ili kupatikana kwayo, kukatazika na kutumia kilevi kwa mara nyingine.

 

            X.          Sharti za kuthibiti adhabu ya kunywa kilevi:

         Haithibiti haddi (adhabu) kwa mtuhumiwa wa unywaji pombe ila kwa mojawapo ya mambo mawili haya:

1)        USHAHIDI KAMILI: Nao ni ushahidi wa watu wanaume wawili waadilifu walio muona akinywa. Wala hauthibiti ushahidi wa mwanaume mmoja na wanawake wawili, wala kwa kujua kadhi (kwamba mtuhumiwa ni mlevi). Na dalili ya hili ni ile hadithi ya Imamu Muslim tuliyo tangulia kuinukuu, katika upigaji mijeledi wa Uthmaan-Allah amuwiye radhi-kumpiga Al-Waleed Ibn Uqbah: (Wakashuhudia dhidi yake wanaume wawili) [1707]

 

2)        IQRAARI (KUKIRI MWENYEWE KUTENDA KOSA: Hili uthibiti kwa mtu kukiri kwamba yeye amekunywa kilevi au tembo. Na Iqraari ni hoja inayo simama mahala pa ushahidi. Na kunatosha kusema katika kukiri kwake: “Nimekunywa kilevi”. Na kunatosha katika ushahidi, kusema mashahidi wawili: “Hakika yeye amekunywa kilevi”.

Wala hakushurutizwi yeye kusema: “Nimekunywa kilevi kwa kujua na kwa khiari”. Au mashahidi wawili kusema: “Amekunywa kilevi ilhali akijua na kwa khiari”. Kwa kuwa asili ni kwamba yeye hakunywa kilevi ila ilhali anajua kuwa ni kilevi na kwa khiari yake akaamua kunywa. Angalia, ikiwa itabainika kwamba yeye alilazimishwa kunywa kwa kutishiwa maisha yake au kwa kunyweshwa. Au ilibainika kwamba yeye hakujua kuwa hilo ni tembo, hakujuzu kumtia haddi. Na dalili ya hilo ni uenevu wa kauli ya Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie: “Hakika Allah ameupomoshea umati wangu kusahau na kukosea na walilo lazimishwa”. Ibn Maajah [2045]-Allah amrehemu.

Wala hayaingii katika hukumu ya cho chote katika ushahidi au Iqraari, matapishi wala harufu inayo toka kinywani. Kwa sababu ya imkani ya kuwepo udhuru, mithili ya kukosea au kulazimishwa. Na kutakapo kuwepo na imkani, hakujuzu kusimamishwa haddi. Haya ni kwa mujibu wa kauli ya Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie: “Waepushieni (waondosheeni) haddi (adabu) kiasi muwezavyo, akiwa na njia (ya kuepuka) basi muachieni. Kwani Imamu kukosea katika kutoa msamaha ni bora kuliko kukosea katika kutoa adhabu”. Abu Daawoud [1424]-Allah amrehemu.

 

         XI.          Anaye tawalia upitishaji/utekelezaji wa haddi:

         Haddi ya unywaji wa kilevi, kama zilivyo haddi nyingine, hakika utekelezwaji wake husimamiwa na kiongozi/mtawala muislamu. Basi lau kiongozi hakuijua kadhia hiyo au hakikuthibiti mbele yake chenye kuwajibisha haddi. Hakujuzu kwa asiye yeye miongoni mwa watu awaami (wa kawaida) kutawalia utekelezaji wa haddi kwa niaba yake, kwa ajili ya kuepuka fitna. Na wala mnywaji wa ulevi au mwenye kustahiki haddi yo yote iwayo, hakalifishwi kujipeleka mwenyewe kwenye haddi mbele ya mahakama. Bali kunamtoshea yeye kutubia toba ya kweli baina yake na Mola wake.

Imepokewa kutoka kwa Anas-Allah amuwiye radhi-amesema: Nilikuwa mbele ya Mtume-Rehema na Amani zimshukie-akajiwa na mtu mmoja, akasema: Ewe Mtume wa Allah! Hakika mimi imenipata haddi, basi nisimamishie. Anasema (mpokezi): Na wala (Mtume) hakumuuliza. Anasema: Ukaingia wakati wa swala, akaswali (jamaa) pamoja na Mtume. Mtume alipo kwisha kuswali, yule mtu akamuinukia, akasema: Ewe Mtume wa Allah! Hakika mimi imenipata haddi, basi nisimamishie (hukumu ya) kitabu cha Allah. (Mtume) akasema: “Hivi wewe hukuswali pamoja nasi?” akajibu: Naam (nimeswali). Akasema: “Basi hakika Allah amekwisha kusamehe madhambi yako”. Au alisema: “Haddi yako”. Bukhaariy [6437] & Muslim [2764]-Allah awarehemu.

Sayyidna Umar-Allah amuwiye radhi-alimwambia mtu mmoja: “Bila ya shaka Allah alikwisha kusitiri lau ungeliisitiri nafsi yako”. Aliitamka kauli hiyo kwenye usikivu wa Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-na wala hakumkanusha. Basi hayo yakafahamisha kwamba haya ndiyo yatakiwayo katika sheria ya Allah Atukukiaye. Mwanadamu aisitiri nafsi yake na atubie baina yake na Mola wake.

Additional information