KARIBU KATIKA MTANDAO WA UISLAMU

"Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui...." 96:1-5

ADHABU ZAMAKOSA YA KITABIA

Kumlazimisha mtu kuwa na tabia njema, hakumfanyi mtu huyo kuwa na tabia njema. Kama ambavyo kumlazimisha mtu kuamini, hakumfanyi mtu huyo kuwa muumini. Kwani uhuru wa nafsi na akili, ndio msingi wa majukumu. Na Uislamu unauheshimu na kuuthamini ukweli huu, nao unajenga fumbulizo la tabia. Ni kwa nini Uislamu utumie nguvu katika kumjuvya mwanaadamu maana ya kheri, au kumuelekeza kuiendea? Na ilhali Uislamu una dhana njema na umbile la mwanaadamu na unaona kuondosha vikwazo vilivyo mbele yake (umbile hilo), kunatosha kuleta kizazi chenye maadili?

 

Naam, ni kweli kwamba umbile la mwanaadamu ni jema, lakini hili halimaanishi kwamba mwanaadamu huyu ni malaika asiye tenda ila kheri/wema tu. Hapana, bali maana yake ni kwamba huo wema unarandana na kukubaliana na umbile lake la asili. Na kwamba huo wema kunaathiri kuukumbatia na kuutenda kwake kama kuruka/kupaa juu kunavyo muathiri ndege. Hivyo ni pindi pale mwanaadamu huyu anapo jinasua na kamba (vizuizi) na mizigo (mazito) yake. Kwa hivyo basi, amali sahihi katika mtazamo wa Uislamu ndio hatua ya mwanzo katika ukataji wa kamba hizo na ondoshaji wa mizigo. Baada ya hapo, mwanaadamu atakapo lemaa/kita katika ardhi na asiweze kutukuka, Uislamu humuona mtu huyo kuwa ni mgonjwa, kisha ndipo humuwepesishia sababu/njia za pozo/shifaa. Na katu Uislamu hautatoa hukumu ya kumtenganisha mwanaadamu huyu na jamii ila tu pale kubakia kwake humo kutakuwa kunachochea shari/uovu kwa wengine. Ni ndani ya wigo wa mipaka hii, ndimo Uislamu unayapiga vita makosa ya kitabia, kwani mwanzo kabisa Uislamu unawajibisha kwamba mwanaadamu aishi katika njia tukufu. Na aishi kwa matunda ya mapambano na juhudi yake ya kweli. Yaani yeye asiujengee uwepo wake juu ya wizi, na ni nini hasa kinacho mpelekea kuiba? Je, ni kule kuhitajia kwake kile kinacho kidhi matashi/matamanio yake? Basi hapo na atoshelezwe kwa mahitaji ya lazima, kiasi cha kumkwasia na kumtoshea na jambo hilo la wizi. Na huo ni wajibu wa jamii, ukilizembea hilo na hivyo kumpelekea mmoja wao kuiba ili kutosheleza mahitaji yake. Basi hapo madhambi ya kosa hilo yanaiangukia jamii iliyo acha kutekeleza wajibu wake na si juu ya yule mwanajamii aliye tupwa.

Angalia, iwapo jamii itautekeleza wajibu wake huu kikamilifu, ikamtoshelezea kila mmoja mahitaji yake ya lazima, kisha baada ya yote hayo akaunyoosha mkono wake kuiba. Hapo kabla ya kutekelezewa adhabu muafaka, itachunguzwa vema hali yake na huko kucheleweshwa kwa adhabu ni jambo litakiwalo kidini. Mpaka kufikia Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-kusema: “Hakika Imamu bila ya shaka kukosea katika kutoa msamaha, ni bora kwake kuliko kukosea katika kutoa adhabu”.

Basi itakapo bainika kutokana na kufuatilia hali za mtu binafsi, kwamba lile umbile lake jema limepondoka/limepogoka na kwamba yeye amekwisha kuwa chanzo cha uadui kwa mazingira (jamii) yaliyo mlea. Na kwamba yeye anaipokea huruma na uangalizi wake (hiyo jamii) kwa kuvunja amani yake na kuchafua usafi wa hali yake. Hapa sasa mazingira/jamii hii haina lawama, itakapo uhukumu uadui wa mmoja wa wanajamii, ikaivunja na kuiharibu silaha ambayo anaitumia kuwaudhi na kuwakera wengine.

Na Qur-ani Tukufu imekwisha ueleza wizi ambao unastahikisha ukataji wa mkono, ya kwamba huo ni wizi wa dhulma na uharibifu. Akasema kumuhusu mwizi muadhibiwa huyu: “LAKINI MWENYE KUTUBIA BAADA YA DHULMA YAKE, NA AKATENGENEA, BASI ALLAH ATAPOKEA TOBA YAKE. HAKIKA ALLAH NI MWENYE MAGHFIRA NA MWENYE KUREHEMU”. [05:39] Utaona kupitia aya hii kwamba adhabu iliyo wekwa na Uislamu, hiyo ni hifadhi ya jamii adilifu tengenefu, dhidi ya madhara/uadui wa mmoja wa wanajamii. Anaye ukabili uadilifu wa jamii yake kwa dhulma na anaupokea utengenefu/wema wake kwa ufisadi/uharibifu.

Huo ni mfano tunao uleta ili kubainisha chini ya kivuli chake kwamba adhabu zitolewazo juu ya makosa ya kitabia. Hazikuwekwa ili kulazimisha maadili mema na kuwashurutisha watu kwa njia ya nguvu, kufuata maadili mema. Kwani njia ya kupigiwa mfano iliyo nayo Uislamu, ni kusema na moyo wa mwanaadamu. Na kuzichochea shauku zake zilizo jificha kuelekea kwenye utukufu (utu) na ukamilifu na kumrejesha kwa Allah Muumba wake Mtukuka kwa muundo/njia ifaayo; yaani kwa kukinaisha na mahaba.

Na ni wajibu kuzitawala hali za mazingira yanayo mzunguka mwanaadamu ili zisaidie kuivisha vipaji vema. Na wala si makosa kuving’oa vimelea visivyo na faida, kwani sisi tuko katika makonde tofauti tofauti ya kilimo. Tunahakikisha ukuaji wa mazao makuu, kwa kung’oa majani na magugu mengi. Kama hivi ndivyo ulivyo umuhimu wa kulinda maslahi ya watu wote. Kwa adhabu za makosa ya jinai zilizo wekwa na kukubaliwa na Uislamu. Adhabu ambazo zimetangulia kutajwa na Taurati na zikazingatiwa kuwa sharia za dini zote za mbinguni.

Uislamu unaibebesha jamii sehemu kubwa ya jukumu la kuelekeza kheri au shari na kueneza maadili mabaya au mema. Na Uislamu kuelekea kwake kutawala nafasi za hukumu, ni kwa sababu ya kutaka kuunda jamii kwa mfumo utakao saidia kujizuia na maovu na machafu na kuwa katika mstari nyoofu.

Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-amepokea kisa cha muuaji aliye taka kutubia madhambi yake na kwamba yeye “Aliuliza mjuzi wa watu wa ardhini, akafahamishwa kwa mwanachuoni mmoja. Akamwambia: Ya kwamba yeye ameua watu mia, basi je anayo toba? Mwanachuoni yule akamwambia: Nenda kwenye nchi kadha, kwani huko kuna watu wanao muabudu Allah, basi nawe muabudu Allah pamoja nao. Na wala usirejee kwenye nchi yako, kwani hiyo ni nchi ya uovu”. Bukhaariy-Allah amrehemu.

Additional information