KARIBU KATIKA MTANDAO WA UISLAMU

"Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui...." 96:1-5

NAMNA YA KUHIJI...inaendelea/2

Na kumesuniwa aende matiti (mbio mbio) katika ile mizunguko mitatu ya kwanza, hivyo ni iwapo Twawaafu hii itaandamiwa na Sa’ayi. Na atembee kawaida katika mizunguko minne iliyo salia na aseme katika kwenda kwake matiti: “ALLAAHUMMAJ-‘ALHU HAJJAN MABRUURAN WADHAMBAN MAGHFUURAN WASA’AYAN MASHKUURAN”. Na kumesuniwa avae rubega (kuacha bega la kulia wazi) katika Twawaafu yote inayo andamiwa na Sa’ayi. Na huku kwenda matiti na kuvaa rubega kunawakhusu wanaume tu, ama mwanamke yeye haendi matiti na wala havai rubega.

 

Na kumesuniwa katika Twawaafu, awe karibu na msikiti mtukufu, kwa kufanya umbali baina yake na msikiti kuwa khatua tatu. Ila kama kuujongelea huko kutamsababishia kero, hapo kuwa mbali ni bora zaidi. Ama mwanamke yeye kumesuniwa kwake awe pembeni kabisa mwa eneo la kutufia iwapo kuna msongamano. Na kumesuniwa kuigusa nguzo – “Al-yamaan” kukimkinika  na kukitomkinika basi atatoshewa kwa kuashiria kwa mbali. Naam, na nguzo za Al-Ka’abah ni nne: Nguzo ile ambayo hapo lipo Hajarul-Aswad, inafuatiwa wakati wa kutufu na nguzo “Al-Iraaqiy”, halafu nguzo “Shaamiy, kisha “Al-Yamaaniy”. Na nguzo hii “Al-Yamaaniy” na ile ambayo hapo lipo “Hajarul-Aswad” ndizo zinazo itwa “Nguzo mbili za Al-Yamaaniy”.

Atakapo maliza kutufu, ataswali rakaa mbili za Sunati-Twawaafu nyuma ya “Maqaamu Ibraahim”, asome katika rakaa ya kwanza [QUL YAA AYYUHAL-KAAFIRUUN] na katika rakaa ya pili [QUL HUWALLAAHU AHAD]. Na baada ya kumaliza kuswali rakaa mbili hizo, aje kulibusu “Hajarul-Aswad” au aliguse  ikiwa inamkinika. Halafu atoke msikitini kwa kupitia mlango wa “Swafaa” kwa ajili ya kufanya “Sa’ayi. Apande kilima Swafaa akianza Sa’ayi, atakapo panda juu ya Swafaa aseme: “ALLAAHU AKBAR ALLAAHU AKBAR ALLAAHU AKBARU WALILLAAHIL-HAMDU, ALLAAHU AKBARU ‘ALAA MAA HADAANAA, WAL-HAMDU LILLAAHI ‘ALAA MAA AULAANAA, LAA ILAAHA ILLAL-LAAHU WAHDAHU LAA SHARIYKA LAHUU, LAHUL-MULKU WALAHUL-HAMDU YUHYII WAYUMIYTU BIYADIHIL-KHAYRU WAHUWA ‘ALAA KULLI SHAIN QADIYR. LAA ILAAHA ILLAL-LAAHU WAHDAU, ANJAZA WA’ADAU, WANASWARA ‘ABDAU, WAHAZAMAL-AHZAABA WAHDAU. LAA ILAAHA ILLAL-LAAHU WALAA NA’ABUDU ILLA IYYAAHU MUKHLISWIYNA LAHUD-DIYNA WALAU KARIHAL-KAAFIRUUN”. Kisha aombe ayatakayo miongoni mwa mambo ya dunia na dini na mwanamume amesuniwa kukariri dua hiyo mara mbili mpaka tatu. Halafu aporomoke kutoka hapo Swafaa atembee mpaka aifikie alama ya kijani, hapo aende matiti mpaka aifikie alama ya pili. Hapo aanze kutembea tena mpaka afike Marwaa, hiyo ni mara moja. Halafu aondoke hapo Marwaa aende zake Swafaa na hiyo ni mara ya pili na ilivyo fardhi khasa ni kufanya Sa’ayi mara saba. Na huko kwenda matiti katika Sa’ayi ni sunah kwa mwanaume, ama mwanamke hakukusuniwa kwake kama ilivyo katika Twawaafu. Na mwenye kufanya Sa’ayi amesuniwa kusema katika Sa’ayi yake: “RABBIGHFIR WARHAM WATAJAAWAZ ‘AMMAA TA’ALAM, INNAKA ANTAL-A’AZZUL-AKRAM”. Na katika darsa zilizo pita imefahamika kwamba lililo wajibu ni kuanzia Swafaa na kukhitimishia Marwaa. Na miongoni mwa mambo ambayo kunafaa kuyazingatia ni kwamba Sa’ayi haitendwi ila baada ya “Twawaaful-Quduum” au “Twawaafu ya nguzo”.

Atakapo maliza kufanya Sa’ayi, akiwa amehirimia Umrah atanyoa au kupunguza nywele zake na hapo atakuwa amemaliza Umrah yake. Na akiwa alihirimia Hijjah hapati tahaluli bali atasalikia kuwa “muhrimu” na atakaa hivyo hivyo Makah mpaka mwezi nane, Mfunguo tatu (Dhul-Hijjah) ambayo ni siku ya “Tarwiyah”. Itakapo fika siku hiyo; siku ya Tarwiyah atahirimia Hijjah kama hakuwa amehirimia. Kisha mahujaji wote wataondoka kuelekea Minaa ili walale hapo usiku huo, asubuhi ya siku ya tisa, baada ya kuchomoza kwa jua mahujaji wataondoka Minaa kuelekea Arafah. Na ilivyo sunah khasa ni Haji kutoingia Arafah ila baada ya kupinduka kwa jua, akae Namirah mpaka baada ya kuingia wakati wa Adhuhuri. Na aswali Adhuhuri pamoja na Laasiri kwa kuzikusanya mjumuisho wa kutanguliza, halafu ndipo aingie Arafah na akae hapo mpaka jua litue. Na hapo Arafah, Haji amdhukuru Mola wake na kumuomba ayatakayo na akithirishe kuleta tahalili. Na afahamu kwamba huko kusimama Arafah ni nguzo inayo mlazimu, kama tulivyo tangulia kueleza. Na zimepokewa dua nyingi za kuombwa katika siku hiyo tukufu kuliko siku zote, miongoni mwa dua hizo ni hizi zifuatazo: “ALLAAHUMMAJ-‘AL FIY QALBIY NUURA, WA FIY SAM’IY NUURA, WA FIY BASWARIY NUURA. ALLAAHUMMASHRAH LIY SWADRIY, WAYASSIR LIY AMRIY”.

“RABBANAA AATINAA FID—DUNYAA HASANATAN WAFIL AAKHIRATI HASANATAN WAQINAA ‘ADHAABAN-NAAR. ALLAAHUMMA INNIY DHWALAMTU NAFSIY DHWULMAN KATHIYRAA WALAA YAGHFIRUD-DHUNUUBA ILLA ANTA. FAGHFIR LIY MAGHFIRATAN MIN ‘INDIKA, WARHAMNIY INNAKA ANTAL-GHAFUURUR-RAHIYM. ALLAAHUMMANQULNIY MIN DHULLIL-MA’ASWIYATI ILAA ‘IZZIT-TWAAH. WAKFINIY BIHALAALIKA ‘AN HARAAMIKA, WA AGHNINIY BIFADHWLIKA ‘AMMAN SIWAAKA, WANAWWIR QALBIY WAQABRIY, WAHDINIY WA AIDHNIY MINAS-SHARRI KULLIHI, WAJMA’A LIYAL-KHAYRA. ALLAAHUMMA INNIY AS-ALUKAL-HUDAA WAT-TUQAA WAL-‘AFAAFA WAL-GHINAA”. Na nyinginezo nyingi, utaziona katika vitabu vya Fiq-hi ukizihitaji.

Jua litakapo tua watakwenda Muzdalifah na kunatosha katika kisimamo cha Arafah, kuhudhuria kitambo cha tangu kupinduka kwa jua mpaka alfajiri ya siku ya Idi. Basi wakati wo wote ndani ya kipindi chote hicho atakao simama Arafah utamtoshelezea kisimamo hicho. Lakini ilivyo bora khasa ni kujumuisha baina ya sehemu ya mchana na ile ya usiku. Haji atakapo fika Muzdalifah, ataswali hapo swala za Maghribi na Ishaa kwa kuzijumuisha mjumuisho wa kuakhirisha na kuziswali rakaa mbili mbili. Na ni wajibu abakie hapo mpaka baada ya nusu ya usiku, iwapo ataondoka kabla ya nusu ya usiku itamuwajibikia damu. Na kumesuniwa aokote Minaa mawe ya kupopolea vinara, nayo ni vikokoto vidogo vidogo. Halafu ataswali alfajiri, kisha aje mpaka asimame “Mash-aril-Haraam”, hili ni jabali dogo lililo mwisho wa eneo la Muzdalifah. Hapo amuombe Allah, na iwe katika jumla ya dua zake: “ALLAAHUMMA KAMAA AUQAFTANAA FIYHI WA ARAYTANAA IYYAAHU, FAWAFIQNAA LIDHIKRIKA KAMAA HADAYTANAA, WAGHFIR LANAA WARHAMNAA KAMAA WA’ADTANAA BIQAULIKA WAQAULUKAL-HAQU: {FAIDHAA AFADHWTUM MIN ‘ARAFAATIN FADHKURULLAAHA ‘INDAL-MASH-ARIL-HARAAM WADHKURUUHU KAMAA HADAAKUM WAIN KUNTUM MIN QABLIHI LAMINAD-DHWAALLIYN. THUMMA AFIYDHWUU MIN HAYTHU AFAADHWAN-NAASU WASTAGHFIRULLAAHA INNAL-LAAHA GHAFUURUR-RAHIYM} Na huko kusimama hapo Mash-aril-Haraam ni sunah.

Inaendelea juma lijalo, inshallaah.

Additional information