KARIBU KATIKA MTANDAO WA UISLAMU

"Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui...." 96:1-5

ALAMA ZA KIYAMA: KUHALALISHWA NA KUKITHIRI UNYWAJI WA POMBE

Alhamdulillah! Himdi zote ni za Allah ambaye hana mwana, wala hana mshirika katika ufalme, wala hana rafiki wa kumsaidia kwa sababu ya udhaifu wake. Na mtukuze kwa utukufu mkubwa. Kisha tumuombe amshushie Rehema na Amani yule aliye Mbora wa wanaadamu wote, yeye pamoja na Aali na swahaba zake wote pia.

 

Ni kwa neema na rehema zake Mola wetu Mkarimu, tunakutana tena juma hili katika jukwaa letu hili, ili tuendelee kuangalia, kusoma na kujifunza Alama miongoni mwa Alama za kukaribia kwa Kiyama kama zilivyo elezwa na Mkweli Muaminifu, lengo kuu likiwa ni kukumbushana ili tupate kujiandaa na siku hiyo. Alama yetu juma hili kama ilivyo elezwa na Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-ni:

 

Kuhalalishwa na kukithiri kwa unywaji wa pombe.

 

 


 

Haya sasa tulihitimishe somo letu hili la leo kwa kuinua mikono ya unyenyekevu na ndimi dhalili tumuombe Mola wetu Mkarimu. Tuombe:

 

رَبَّنَا ٱغۡفِرۡ لِي وَلِوَٰلِدَيَّ وَلِلۡمُؤۡمِنِينَ يَوۡمَ يَقُومُ ٱلۡحِسَابُ ٤١

 

Mola wetu! Unighufirie mimi na wazazi wangu wote wawili, na Waumini, siku ya kusimama hisabu”. Ibrahim [14]:41

 

Mola wetu Mtukufu kwa rehema zako tunakuomba utupe Amani na Salama katika:

 

يَوۡمَ لَا يَنفَعُ ٱلظَّٰلِمِينَ مَعۡذِرَتُهُمۡۖ وَلَهُمُ ٱللَّعۡنَةُ وَلَهُمۡ سُوٓءُ ٱلدَّارِ ٥٢

 

Siku ambayo hautawafaa madhaalimu udhuru wao na watapata laana, na watapata makaazi mabaya kabisa”. Ghaafir [40]:52

 

Aamina!

 

Jukwaa letu juma hili linatamatia hapa, tunamshukuru Allah Mola Muumba wetu kwa haya aliyo tuwezesha kukuletea katika jukwaa letu na tunataraji yatakuwa yanazidi kukusogeza karibu zaidi na Mola wako na kwamba unauona ukaribu wa siku hiyo ngumu inayo tujongelea. Juma lijalo kwa uweza wake Mola tutaendelea kujifunza alama nyinginezo kama zilivyo elezwa na Yule Mkweli Muaminifu ambaye:

 

وَمَا يَنطِقُ عَنِ ٱلۡهَوَىٰٓ ٣ إِنۡ هُوَ إِلَّا وَحۡيٞ يُوحَىٰ ٤

 

Wala hatamki kwa matamanio. Hayakuwa haya (ayatamkayo) ila ni ufunuo (wahyi) ulio funuliwa”. An-Najmi [53]:03-04

 

Allah ndiye Muwezeshaji Wetu Mkuu.

 

Tukutane juma lijalo katika muendelezo wa makala zetu hizi, in shaa Allah.

 


 


 


 

Additional information