|
xi.
Kuvua katika talaka:
Kama inavyo swihi talaka iliyo angikwa juu ya sifa
fulani au sharti fulani, ndivyo inavyo swihi talaka iliyo ingiwa na uvuaji. Na
muradi/makusudio ya kuvua katika talaka: Ni mume kukusanya zaidi ya talaka moja
kwa tamko moja, kisha anatoa baadhi yake kwa kutumia ala/chombo cha kuvua,
ambacho ni herufi “ILA”, kwa kusema kumwambia mke wake: “Wewe umeachwa talaka
tatu, ILA talaka moja”, hapa ataachika talaka mbili. Au akamwambia: “Wewe
umeachwa talaka tatu, ILA mbili”, hapa atakuwa ameachika talaka moja.
Kuswihi kwa talaka ya kuvua, ni kwa sababu uvuaji (Istithnaa)
wa kinacho hesabiwa, ni muundo/mtindo lugha wa Kiarabu unao fuatwa (tumiwa)
na umetumiwa na Qur-ani na Sunna (Hadithi) katika kuelezea maana mbali mbali na
kudhibiti kiasi na idadi. Allah Ataadhamiaye amesema akihadithia juu ya Nabii
Nuhu-Amani imshukie: “NA HAKIKA TULIMTUMA NUHU KWA WATU WAKE, NA AKAKAA NAO
MIAKA ELFU ILA (kasoro) MIAKA KHAMSINI...” [29:14]
Kwa ajili/sababu ya kutumiwa kwake na Qur-ani, ndio kumejuzu
kutumia uvuaji katika kuielezea talaka na kudhibiti idadi ya talaka zilizo
kusudiwa kutolewa.
xii.
Sharti za kuswihi kuvua
katika talaka:
Ili uvuaji katika talaka uswihi, kumeshurutizwa
kuchunga masharti yafuatayo:
1.
Mtoa talaka (mume) anuie kuunganisha
uvuaji na maneno ya asili yenye kuvuliwa. Lau atakamilisha kutamka maneno yake
ya asili, kisha ikampitikia akilini mwake kuvua sehemu/baadhi yake, hakutoswihi
kuvua huko na talaka itatuka kama inavyo hukumiwa na maneno yake asili kabla ya
kuyatundikia uvuaji.
2.
Tamko la kuvua liungane na tamko lenye
kuvuliwa kwa kufuata ada ya mahala husika.
Angalia, lau atatenganisha baina ya matamko mawili hayo; lenye
kuvua na lile lenye kuvuliwa, kwa kitambo kinacho zingatiwa na ada kuwa ni
kitenganishi, kama vile dakika moja mathalan, uvuaji wake huo utakuwa ni batili.
Na talaka itatuka kwa mujibu wa mahukumio ya tamko lenye kuvuliwa. Sura yake ni
mume kumwambia mke wake: “Nimekuacha talaka tatu”, kisha akanyamaza kidogo
halafu ndipo akasema: “ILA talaka moja/mbili”.
3.
Uvuaji usizamishe (usilingane/usizidi)
kiasi/idadi ya kile kinacho vuliwa, kama vile kusema: “Nimekuacha talaka tatu
ILA tatu”. Uvuaji kama huu, huzingatiwa kuwa ni puo (upuuzi) na hukumu itabakia
kwa vile inavyo hukumiwa na tamko vuliwa; yaani hizo zitakuwa ni talaka tatu.
Baada ya hayo, sasa unapaswa kufahamu kwamba uvuaji katika
maneno ya kukubali, huzingatiwa kuwa ni kukanusha. Na uvuaji katika maneno ya
kukataa, huzingatiwa kuwa ni kuthibitisha, kwa sababu uvuaji hupewa kinyume cha
hukumu ya asili ya chenye kuvua. Lau kama mume atasema: “Sikukuacha ILA talaka
mbili”, zitakuwa talaka mbili.
xiii.
Dalili ya kuswihi kuvua
katika talaka:
Dalili ya kuswihi kuvua katika talaka, ni kauli ya
Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie: “Atakaye acha huru mtumwa au
akaacha mke na akavua, kunamuelea kuvua kwake huko”. Ibn Al-Athiyr
[AN-NIHAAYAH]
xiv.
Kumkabidhi mke mamlaka ya
kujiacha:
Kunaswihi mume kuyahamisha mamlaka ya kutoa talaka
kutoka kwake kwenda kwa mke wake. Na uhamishaji huo, huwa katika daraja ya
kummlikisha mke talaka.
xv.
Sharti za kutuka kwa talaka
milikishwa:
Ili talaka ya namna hii iswihi, kumeshurutizwa
kupatikana kwa sharti zifuatazo:
1.
Talaka hiyo iwe ni ya kutinda (kukata),
kwani hakuswihi kuitundika juu ya kitu/jambo fulani. Hivi ni kama vile mume
kumwambia mke: “Ikifika kesho, basi jiache”.
2.
Mume mmilikishi talaka awe ni mukalafu
(mtu mzima, mwenye akili timamu), kwani hauswihi umilikishi talaka wa mume mtoto
au mwenda wazimu.
3.
Mke mmilikishwa pia awe mukalafu, kwani
hauswihi umilikishwaji talaka wa mke mtoto au mwenda wazimu.
4.
Mke ajiache haraka mara tu baada ya
kupewa mamlaka ya kujiacha, kwani lau atakuchelewesha huko kujiacha kwa kitambo
kinacho likata tamko la “Qabuul” na “Ijaabu” ya ndoa, talaka hiyo haitaswihi.
xvi.
Dalili ya kujuzisha
kumkabidhi mke mamlaka ya kujiacha:
Hutolewa dalili ya kujuzisha kummilikisha mke talaka,
kile kitendo cha Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-cha kuwapa khiari wake
zake wachague ama kuendelea kuishi naye au kuachwa. Na hilo ni pale ilipo shuka
kauli yake Allah Ataadhamiaye: “EWE NABII! WAAMBIE WAKE ZAKO: IKIWA MNATAKA
MAISHA YA DUNIA NA PAMBO LAKE, BASI NJOONI, NITAKUPENI KITOKA NYUMBA, NA
KUKUACHENI MWACHANO MZURI”. [33:28]
Lau
kuchagua kwao kuachwa kusingeli kuwa na athari yoyote, basi kule kupewa kwao
khiari ya kuchagua, kusingeli kuwa na maana yoyote.
|