KARIBU KATIKA MTANDAO WA UISLAMU

"Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui...." 96:1-5

DONDOO ZA WIKI

VITA VYA AHZAABU (KHANDAQ)

 Mapenzi ya kuangamiza ndiyo yaliyowasukuma Mayahudi  kukusanya makundi (Ahzaabu) ya Waarabu dhidi ya Mtume na maswahaba wake.

       Nafsini mwa Banin-Nadhwiyr suala la kutolewa na kufukuzwa Madinah halikuwa ni jambo jepesi hata kidogo kiasi cha kuachwa lipite hivi hivi tu. Wala halikuwa ni jambo lenye kukoma athari zake kwa kumalizika kwake. Haikuwa hivyo kwa sababu Madinah ndio palikuwa mahala pao na mahala pa wahenga wao kwa karne kadhaa.

Endelea

HUKUMU ZA SHERIA KATIKA MAS-ALA YA KUZUIA MIMBA...INAENDELEA

Hakumjuzii mwanamume kufanya upasuaji wa kufunga kizazi (vassectomy) ila kwa dharura. Na kutokuwa na raghba (mapenzi-matashi) ya kuzaa, hakuuhalalishi upasuaji huo na hiyo ni mojawapo ya aina za kumtia mtu utasa ambao hakuumbwa nao.

7)        Hakumjuzii mwananmume kujifanya maksai kwa kuvunjwa pumbu kama kusivyo mjuzia kuikata dhakari yake. Kwani yote hayo ni kulibadilisha umbile la Allah bila ya kuwepo maslahi ya kisheria au dharura – lazimishi. Na isitoshe kufanya hivyo ni kuiadhibu nafsi na kuharibu manufaa ya kiungo bila ya kuwa na sababu – kubalishi kisheria.

Endelea

AMALI ZINAZOWANUFAISHA WAZAZI BAADA YA KUFA

Imepokewa kutoka kwa Maalik Ibn Rabeeah As-saaidiy-Allah amuwiye radhi-amesema: "Wakati mmoja tukiwa tumekaa mbele ya Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-tahamaki akajiwa na mtu mmoja wa kabila la Salamah, akasema: Ewe Mtume wa Allah! Je, bado ninawiwa na wema wa kuwatendea wazazi wangu baada ya kufa kwao? (Mtume) akajibu: "Naam, kuwaombea dua na maghufirah, kutekeleza ahadi zao baada ya (kufa) kwao,kuunga udugu ambao hauungwi ila kwa kupitia kwao na kumtukuza (kumuheshimu) rafiki yao". Abu Daawoud & Ibn Maajah-Allah awarehemu.

Endelea

ADHANA ISIYO YA SWALA

Kumesuniwa kutolewa adhana pindi kutakapotokea katika jamii ya waislamu mambo kadhaa mbali ya swala. Mambo hayo yaliyosuniwa adhana ni pamoja na:-

Kumuadhinia mtoto katika sikio lake la kulia mara tu baada ya kuzaliwa, kama ambavyo ni suna kuleta iqaamah katika sikio lake la kushoto.

Suna hii inatokana na kitendo cha Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-kumuadhinia sikioni mjukuu wake; Hassan alipozaliwa na Bibi Faatimah (bintiye). Riwaya hii ameipokea imamu Tirmidhiy

Endelea

Additional information